Kuweka Dhikr ya kwenye Rukuu´ katika Sujuud na kinyume chake

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumwambia aseme:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika  Mola wangu, Aliye juu kabisa, kutokamana na mapungufu yote.”

Je, hakuna chochote kinachomlazimu mwenye kuweka:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

mahali pa:

سبحان ربي الأعلى

“Ametakasika  Mola wangu, Aliye juu kabisa, kutokamana na mapungufu yote.”?

Jibu: Hapana. Imepokelewa katika dalili zingine. Maandiko yanatakiwa kuoanishwa. Imepokelewa katika matendo yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Isitohe amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Imepokelewa pia katika baadhi ya mapokezi kwamba akirukuu aseme:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23763/حكم-قول-ذكر-الركوع-في-السجود-والعكس
  • Imechapishwa: 22/04/2024