Hukumu ya kuomba du´aa katika Rukuu´

Swali: Je, inafaa kuomba du´aa katika Rukuu´ kama ilivyo katika Sujuud?

Jibu: Katika Rukuu´ kuna matukuzo:

“Ama Rukuu´ mtukuzeni Mola.”

Hata hivyo kuomba du´aa yenye kuandamana haina neno:

سبحانك اللهم ربنا وبحمدك اللهم اغفر لي

“Ametakasika, Mola wetu, himdi zote ni Zake. Ee Allaah! Nisamehe.”

Du´aa hii ni yenye kuandamana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ama Rukuu´ mtukuzeni Mola. Ama Sujuud jitahidini katika kuomba du´aa.”

Swali: Kwa msemo mwingine ni kwamba asiombe jambo lolote la kilimwengu?

Jibu: Hapana. Amtukuze Mola:

سبحان ربي العظيم

“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”

سبحانك اللهم ربنا وبحمدك اللهم اغفر لي

“Ametakasika, Mola wetu, himdi zote ni Zake. Ee Allaah! Nisamehe.”

سبوح قدوس رب الملائكة والروح

“Umetakasika sana kutokamana na mapungufu na uchafu; Mola wa Malaika na roho!”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23765/ما-حكم-الدعاء-في-الركوع
  • Imechapishwa: 22/04/2024