Swali: Tunaona kwenye makaburi ya waislamu hii leo wanaweka nguzo ndefu kama vile mti, mfuko mkubwa au sanduku lenye rangi kama alama anapokuja kutembea. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Mambo haya yanaweza kuingia katika yale makaburi yaliyonyanyuliwa na yaliyo waziwazi. Ni mambo yasiyotakiwa. Kinachotakiwa ni mtu atosheke na kitu kidogo tu anachoweza kufanya kama alama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (11) http://binothaimeen.net/content/6742
  • Imechapishwa: 27/11/2020