13 – Wivu

Moja katika sifa za mwanamke ni wivu. Inasemekana kuwa mwanamke ana wivu zaidi kuliko mwanaume. Mwanamke mwenye wivu bila ya sababu atateseka na matatizo mengi yasiyokuwa na kikomo.

Miongoni mwa wivu usiokuwa na sababu ni kufuatilia mienendo mbalimbali ya mume. Anakuwa ni mwenye kumfanyia hesabu na anakuwa ni kama vile mshuma na taa wakati anapoingia, wakati anapotoka, anaposhika simu, anapoandika meseji na anapozima simu anakuwa ni mwenye kumchunga. Huu sio wivu, huu ni ugonjwa. Hapo ndipo unapotea uaminifu kati yao. Unapopotea uaminifu na mapenzi yakaondoka, basi hakuna kilichobaki isipokuwa kuachana.

Maisha haya yana faida gani kunapokosekana moja katika hivi vitatu:

1 – Uaminifu.

2 – Mapenzi.

3 – Mahaba.

Hakuna kitu. Hivyo mwanamme analazimika kumtuma kwa familia yake na hali yake mume inaeleza kuwa anamchunga, anampa dhiki na hana uaminifu naye. Nini ninachotaraji kwake?

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 13/04/2024