18. Sababu ya kumi na nne ya talaka ambayo ni mke kumpelekesha mume

14 – Mke mwenye kummiliki mume

Mume anayeitwa kuwa ni mwenye kumtawala mume na ambaye anapenda ule umiliki wa ziada na kumtawala mume wake na maisha yake. Jambo hili pia linaingiwa na wasiwasi. Mwanamke huyu pia hataki mumewe ampende mwingine zaidi yake mpaka huwa anakasirika anapomuona mume anamfanyia wema mama yake, anamfanyia huruma, anamtekelezea matakwa yake, au anawaonea huruma ndugu na dada zake, anakasirishwa na jambo hilo na kumtawala. Hataki ampende wala kumhurumia mwingine zaidi yake. Anachotaka ni mume wake kujisalimisha kwake yeye tu na yeye mwanamke ndiye anayetaka kumpelekesha. Mfano wa mwanamke kama huyu akiendelea na hali hii basi kuna uhakika mkubwa kwa mume kumtaliki.

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 33
  • Imechapishwa: 14/04/2024