Amesema (´Azza wa Jall):

وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ

”Siku itakayosimama Saa wataapa wahalifu kuwa hawakubakia isipokuwa saa moja tu; hivo ndivyo walivyokuwa wakizua.”[1]

يَتَخَافَتُونَ بَيْنَهُمْ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا

”… wakinong’onezana kati yao: ”Hamkukaa isipokuwa siku kumi tu.”[2]

نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذْ يَقُولُ أَمْثَلُهُمْ طَرِيقَةً إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا

”Sisi Tunajua zaidi yale wanayoyasema; atakaposema mbora wao katika kuigwa: ”Hamkukaa isipokuwa siku moja tu!”[3]

يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا

”… Siku atayokuiteni, nanyi mtamuitika na huku mkimuhimidi, na mtaona kama vile hamkubakia isipokuwa kitambo kidogo tu.”[4]

Kwa ajili hiyo mazanadiki wakatia mashaka.

Kuhusu maneno Yake:

يَتَخَافَتُونَ بَيْنَهُمْ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا

”… wakinong’onezana kati yao: ”Hamkukaa isipokuwa siku kumi tu.”,

kunakusudiwa pale watapotoka kwenye makaburi yao. Watayaona yale yanayohusiana na Ufufuliwaji ambayo walikuwa wanayakadhibisha. Wataambizana kuwa hawakukaa kwenye makaburi isipokuwa siku kumi. Kisha baada ya hapo wataona kuwa siku kumi ni ndefu, ndio watasema:

إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا

”Hamkukaa isipokuwa siku moja tu!”[5]

Bi maana ndani ya makaburi. Kisha baada ya hapo wataiona hata siku moja hiyo kuwa ndefu, ambapo wataambiana kuwa hawakukaa isipokuwa kitambo fulani cha mchana. Hiyo ndio tafsiri ya yale waliyoyatilia mashaka mazanadiki[6].

[1] 30:55

[2] 20:103

[3] 20:104

[4] 17:52

[5] 20:104

[6] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 14/04/2024