12. Hapa ndipo Mitume watasema kuwa hawajui chochote

Katika Aayah moja Amesema:

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ

“Siku Allaah atawakusanya Mitume na kuwaambia: “Mlijibiwa nini?” Watasema: “Hatuna ujuzi nalo, kwani hakika Wewe unayajua mno yenye kufichikana.”[1]

Katika Aayah nyingine Amesema:

وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ

”… mashahidi watasema ”hawa ndio wale waliomzulia uwongo Mola wao!””[2]

Wanauliza kwamba ni vipi wanasema ”hawajui”, kisha kwamba ”hawa ndio waliomsemea uwongo Mola wao”. Wakadai kuwa Qur-aan ni yenye kujigonga.

Kuhusu maneno Yake:

يَوْمَ يَجْمَعُ اللَّـهُ الرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَا أُجِبْتُمْ ۖ قَالُوا لَا عِلْمَ لَنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّامُ الْغُيُوبِ

“Siku Allaah atawakusanya Mitume na kuwaambia: “Mlijibiwa nini?” Watasema: “Hatuna ujuzi nalo, kwani hakika Wewe unayajua mno yenye kufichikana.”

atawauliza pale Moto utapopumua. Atawauliza walijibu vipi juu ya upwekeshaji, akili yao ipotee wakati Moto utakapotoa pumzi na waseme:

لَا عِلْمَ لَنَا

“Hatuna ujuzi nalo… ”

Kisha baadaye fahamu yao irudi na waseme:

هَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ

”… hawa ndio wale waliomzulia uwongo Mola wao”

Hii ndio tafsiri ya yale waliyoyatilia mashaka mazanadiki[3].

[1] 5:109

[2] 11:18

[3] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 74-76
  • Imechapishwa: 14/04/2024