13. Kipindi ambapo Allaah haonekani na wakati anapoonekana

Amesema:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ

“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri. Zikimtazama Mola wake.”[1]

Amesema katika Aayah nyignine:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki bali Yeye anayazunguka macho yote.”[2]

Wanauliza inakuweje. Kwanza anasema kuwa wanamtazama Mola wao, kisha katika Aayah nyingine anasema:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki bali Yeye anayazunguka macho yote.”

Wakaitilia shaka Qur-aan na wakadai kuwa ni yenye kujigonga.

Kuhusu maneno Yake:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاضِرَةٌ

“Kuna nyuso siku hiyo zitanawiri… ”

kunalengwa kwa uzuri na weupe. Na maneno Yake:

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ

“… zikimtazama Mola wake.”

bi maana zinamwangalia Mola wao kwa macho yao. Kuhusu maneno Yake:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki bali Yeye anayazunguka macho yote.”[3]

ni duniani na si Aakhirah. Hapo ni pale ambapo mayahudi walimwambia Muusa:

أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً

”Tuonyeshe Allaah waziwazi.”[4]

Watapoteza fahamu na wakaadhibiwa kutokana na maombi yao. Na wakati washirikina wa Quraysh walipomuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

أَوْ تَأْتِيَ بِاللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا

”… au umlete Allaah na Malaika uso kwa uso.”[5]

Allaah (Ta´ala) akasema:

أَمْ تُرِيدُونَ أَن تَسْأَلُوا رَسُولَكُمْ كَمَا سُئِلَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ

”Au mnataka kumuuliza Mtume wenu kama alivyoulizwa Muusa hapo kabla?”[6]

Bi maana pale waliposema:

أَرِنَا اللَّـهَ جَهْرَةً

”Tuonyeshe Allaah waziwazi.”[7]

Ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki bali Yeye anayazunguka macho yote.”

Bi maana hakuna yeyote mwenye kumuona duniani tofauti na Aakhirah. Aayah inakusudia duniani. Kuhusu Aakhirah watamuona. Hiyo ndio tafsiri ya yale waliyoyatilia mashaka mazanadiki[8].

[1] 75:22-23

[2] 6:103

[3] 6:103

[4] 4:153

[5] 17:92

[6] 2:108

[7] 4:153

[8] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 76-78
  • Imechapishwa: 14/04/2024