Swali: `Allaamah Ibn-ul-Qayyim amesema:

“Kuna sampuli mbili za nyuchi:

1 – Uchi mkubwa

2 – Uchi mwepesi.

Akajumuisha mapaja miongoni mwa uchi mwepesi?

Jibu: Hapana shaka kuwa tupu ya nyuma na ya mbele ni katika nyuchi kubwa. Mapaja yanalinda ule uchi mkubwa. Maoni ya sawa ni kwamba ni uchi. Hadiyth tatu zinatiana nguvu; Hadiyth ya Muhammad bin Jahsh, Jarhad na Ibn ´Abbaas. Zinatiana nguvu na hivyo zinafuta yale yaliyomtokea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Ambaye anavaa kaptula na nguo nyepesi?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Ni lazima kufunika mapaja.

Swali: Mtoto wa kiume anatakiwa kufunika mapaja?

Jibu: Akishabaleghe. Salama na bora zaidi afunike mapaja akiwa ni mtoto wa miaka kumi na mfano wake. Isitoshe kunamuweka mbali zaidi na mtihani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23721/حكم-ستر-الفخذين-للكبير-والصغير
  • Imechapishwa: 14/04/2024