´Umrah zaidi ya mara moja ndani ya mwezi mmoja

Swali: Je, inafaa kukariri ´Umrah zaidi ya mara moja ndani ya mwezi na ni ipi dalili ya hilo?

Jibu: Mwekaji Shari´ah (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) hakuweka kikomo chochote baina ya ´Umrah mbili. Wala haikuthibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliweka kikomo cha kitu. Yeyote ambaye ataweka kikomo basi alete dalili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”´Umrah hadi ´Umrah nyngine ki kifutio cha madhambi kwa yale yaliyoko kati yake na hajj yenye kukubaliwa haina malipo mengine zaidi ya Pepo.”

Hakuweka kikomo chochote. Dalili ataombwa yule ambaye ataweka kikomo na si kutoka kwa yule ambaye hakuweka kikomo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4778/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D8%AA%D9%83%D8%B1%D8%A7%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%85%D8%B1%D8%A9-%D9%81%D9%8A-%D8%B4%D9%87%D8%B1-%D9%88%D8%A7%D8%AD%D8%AF
  • Imechapishwa: 27/11/2020