Abu Nu´aym ´Abdul-Malik bin al-Hasan al-Isfaraayiyniyn, mtoto wa dadake Abu ´Awaanah, amesema:

“Nilimsikia baba yangu akisema kumwambia Haafidhw Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy: “Wakati mimi na Abu ´Awaanah tulipofika Baswrah tukasikia kwamba Abu Khaliyfah amekatwa na anatuhumiwa kwamba anasema kuwa Qur-aan imeumbwa.” Abu ´Awaanah akanambia: “Ee mwanangu! Ni lazima tukutane naye.” Baada ya kitambo Abu ´Awaanah akamwambia: “Unasemaje juu ya Qur-aan?” Uso wake ukapiga wekundu na akanyamaza. Kisha akasema: “Qur-aan ni maneno ya Allaah na hayakuumbwa. Yule mwenye kusema kuwa imeumbwa ni kafiri. Mimi natubu kwa Allaah juu ya kila dhambi isipokuwa tu uongo, kwani mimi kamwe sijawahi kusema uongo. Namuomba Allaah msamaha.” Abu ´Aliy akasimama na akaenda kubusu kichwa cha baba yangu. Baba yangu akasema: “Abu ´Awaanah akasimama na kwenda kubusu mabega ya Abu Khaliyfah.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/10)
  • Imechapishwa: 27/11/2020