Kuwatembelea wazazi makaburini siku ya ijumaa na kutembea peku

Swali: Baadhi ya Shiy´ah wanaenda kwenye makaburi na wanaketi chini na anakuwepo mtu anayezungumza na wanalia pamoja na wanamme na wanawake.

Jibu: Shiy´ah hawafuatwi. Shiy´ah Raafidhwah ni wenye kuchupa mipaka kwa wafu na ni wenye kupinduka mipaka kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo hawaigwi. Sunnah ni wewe kusimama, kuwatolea salamu na kuondoka zako. Hapana vibaya akiwa si muweza wa kusimama akaketi chini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliketi chini karibu na kaburi la mama yake na akamuombea du´aa mpaka alipokatazwa jambo hilo.

Swali: Baadhi ya ambao wanayatembelea makaburi – kama vile mtu kuwatembelea wazazi wake – wameifanya maalum siku ya ijumaa na wanaenda kwenye kaburi na wanaketi karibu nalo. Pengine asiombe du´aa na akaketi hapo kwa kitambo.

Jibu: Jambo hili halina msingi. Kuifanya maalum siku ya ijumaa hakuna msingi. Kuyatembelea makaburi kunakuwa siku yoyote.

Swali: Mtu anatakiwa kutembea peku pale wakati anapoingia makaburi au pale kati ya makaburi?

Jibu: Kati ya makaburi peke yake. Hapana vibaya kabla yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22320/ما-المشروع-في-زيارة-القبور-ووقتها-وادابها
  • Imechapishwa: 05/02/2023