Swali: Je, du´aa yenye kukubaliwa inabadilisha kitu?

Jibu: Hapana, haibadilishi kitu. Kila kitu kinatembea kwa mujibu wa makadirio yake yaliyotangulia. Yaliyotimia yamekwishatimia na yaliyotundikwa yamekwishatundikwa. Kuna makadirio ambayo yametundikwa na kuna makadirio ambayo yamekwishatimia. Mtu anatakiwa kumuomba Mola Wake. Kwani hakika Yeye ni Mwingi wa hekima, Mjuzi wa yote (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22323/هل-الدعاء-المستجاب-يغير-ما-هو-مقدر
  • Imechapishwa: 05/02/2023