Anamuomba Allaah ufalme usiyomalizika

Swali: Namshuhudisha Allaah kwamba mimi nakupenda kwa ajili Yake. Ni ipi hukumu ya kuomba du´aa ifuatayo:

اللهم يا مالك الملك، تُؤتي الملك من تشاء، وتنزع الملك ممن تشاء، أسألك مُلكًا لا يَفْنَى

”Ee Allaah, ee Mfalme wa wafalme! Hakika Wewe unampa ufalme umtakaye na unamwondolea ufalme umtakaye. Hivyo basi, nakuomba ufalme usiyomalizika.”?

Swali: Kuhusu kupenda kwa ajili ya Allaah ni miongoni mwa ´ibaadah zinazomkurubisha mtu kwa Allaah. Hivyo basi, nami nasema “Akupende Allaah ambaye umenipenda kwa ajili Yake”.

Kuhusu ufalme duniani itambulike kuwa hakuna ufalme usiyomalizika. Lakini ni sawa iwapo amekusudia Pepo. Ama ikiwa anakusudia ufalme wa duniani usiyomalizika si sahihi. Dunia yote ni yenye kuteketea:

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانِ

”Kila aliyekuwa humo [mbinguni na ardhini] atatoweka.”[1]

Lakini ni sawa endapo anakusudia ufalme huko Aakhirah. Kwa maana nyingine Peponi.

Swali: Kwa hivyo kuomba hivo kunaingia katika kuchupa mpaka katika du´aa?

Jibu: Ndio.

[1] 55:26

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22318/ما-حكم-سوال-الله-ملكا-لا-يفنى
  • Imechapishwa: 05/02/2023