Kunyanyua mikono wakati wa kumuombea maiti II

Swali: Vipi kuhusu kunyanyua mikono mbele ya kaburi wakati wa kumuombea maiti?

Jibu: Hapana vibaya. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema kuwa wakati (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoyatembelea makaburi alinyanyua mikono yake.

Swali: Alifanye kaburi kuwa kati yake yeye na Qiblah?

Jibu: Upande wowote. Wigo ni mpana katika jambo hili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22319/حكم-وكيفية-الدعاء-عند-القبر
  • Imechapishwa: 04/02/2023