Kuwapa malezi mema watoto wako ni muhimu zaidi kuliko biashara

Swali: Unajua kuwa baadhi ya wazazi wameshughulishwa na kazi zao na wanakuwa si wenye kuwauliza watoto wao wa kike maendeleo yao ya masomo au ni kina nani wanaotangamana nao. Je, huku ni kupoteza haki zao?

Jibu: Kusema kwamba wameshughulishwa na kazi zao, tunasema kwamba kazi yake kubwa alionayo ni watoto wake wa kiume na wa kike. Majukumu yao ni makubwa kuliko majukumu alionayo ya biashara yake. Tunamuuliza ni kipi anachotaka katika biashara yake? Hakuna kingine anachotaka isipokuwa kujihudumia yeye na familia yake. Hiki uangalizi wa miili. Muhimu kuliko hilo ni uangalizi wa moyo, roho, kuiimarisha imani na matendo mema kwenye nafsi za watoto wa kiume na wa kike. Kitu kingine kinachotakiwa kutambulika ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake yote yanakatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea.”

Mtoto mwema anamnufaisha baba na mama yake maishani na wakati wa kufa. Kwa hivyo ana haki zaidi kuliko uangalizi wa mali. Mali ikiwa yule mwenye kuimiliki ni mwenye utajiri mkubwa basi anaweza kuajiri wafanyikazi wakaifanyisha biashara. Ikiwa ni chini ya hapo basi Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia njia ya kutokea.” (65:02-03)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1313
  • Imechapishwa: 29/06/2020