Swali: Sauti haiko wazi na tumechoweza kusikia tu ni kama inajuzu kwa muislamu kuwaombea wazazi wake ambao ni makafiri…

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kuwaombea du´aa wazazi wawili ambao ni makafiri wala kuwaombea msamaha. Allaah (Ta´ala) Amesema:

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee msamaha washirikina, japokuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.” (09:113)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuomba idhini Mola Wake kutembelea kaburi la mama yake, Allaah Akampa idhini na akawa ameenda kumtembelea. Halafu baada ya hapo akamuomba idhini ya kumuombea msamaha, Allaah Akamkataza. Allaah Alimkataza kumuombea du´aa mama yake. Hii ni dalili inayoonesha kuwa muislamu hamuombei msamaha kafiri hata kama atakuwa ni baba yake au mama yake:

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee msamaha washirikina, japokuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.”

Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwambia ami yake Abu Twaalib kuwa atamuombea msamaha midhali hajakatazwa, ndipo Allaah Akateremsha Aayah hii:

مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَابُ الْجَحِيمِ

“Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombee msamaha washirikina, japokuwa ni jamaa zao wa karibu, baada ya kuwabainikia kwamba wao ni watu wa Motoni.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1430-7-20.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2015