Kuwafutarisha masikini na wasiokuwa masikini

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kumfutarisha mfungaji basi anapata mfano wa ujira wake pasi na kupungua chochote katika zile thawabu za mfungaji.”[1]

Je, hilo linawahusu mafukara peke yao au linawahusu matajiri na wengineo?

Jibu: Udhahiri wa Hadiyth ni kuenea. Hakufanya maalum kwa kuwafutarisha mafukara. Kuwafutarisha wafungaji ni kujikurubisha na kumtii Allaah (Ta´ala). Hata hivyo mafukara ni wahitaji zaidi juu ya jambo hilo. Mafukara wanahitaji zaidi jambo hilo. Ni sawa akiwafutarisha ndugu zake katika jamaa na majirani zake ijapo watakuwa matajiri. Katika kufanya hivo kuna kusaidiana, kumtendea wema jirani, jamaa na kuunga kizazi. Ndani yake kuna manufaa mengi. Hadiyth ni yenye kuenea na inamkusanya tajiri, fukara, ndugu na wengineo.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1078)”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 01/04/2023