Pindi Maghrib inakusanywa na ´Ishaa katika Ramadhaan

Swali: Hali ya Tarawiyh inakuweje pindi kunapokusanywa kati ya Maghrib na ´Ishaa katika Ramadhaan?

Jibu: Itaswaliwa baada ya ´Ishaa. Maghrib ikikusanywa na ´Ishaa katika wakati wa Maghrib kutaswaliwa Tarawiyh [baada yake]. Ikiwa ni ndani ya Ramadhaan wakati wa swalah ya Tarawiyh, Raatibah ya ´Ishaa, Sunnah ya Maghrib na Sunnah ya ´Ishaa ataziswali baada ya ´Ishaa. Hapana neno pia akileta Witr kwa sababu Witr na Tahajjud inakuwa baada ya ´Ishaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 01/04/2023