Kuwadumia mahujaji na kueneza elimu ni katika njia ya Allaah

Swali: Kuwahudumia mahujaji kama vile kuwapa chakula na mahitaji mengine ni katika njia ya Allaah?

Jibu: Katika njia ya Allaah maana yake ni katika kumtii Allaah. Sio kama jihaad. Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa hajj ni katika njia ya Allaah. Kwa sababu imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba bwana mmoja katika Wanusuraji aliacha anausia ngamia wake atumiwe katika njia ya Allaah ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia mke wake:

“Hiji kwa kumtumia, kwani hakika hijjah ni katika njia ya Allaah.”

Kunatarajiwa juu yake kheri kubwa.

Swali: Je, kunaingia pia kujitolea baadhi ya vijitabu au kanda zenye manufaa?

Jibu: Ndio, kunatarajiwa juu yake kheri. Kwa sababu ni katika kufikisha elimu. Kanda, Khutbah na vitabu zote ni njia za kufikisha elimu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22909/هل-الانفاق-على-الحجاج-يعد-في-سبيل-الله
  • Imechapishwa: 12/09/2023