16. Ni kipi cha kwanza kilichomteremkia Mtume katika Qur-aan?

Swali 16: Ni kipi cha kwanza kilichomteremkia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Qur-aan?

Jibu: Cha kwanza kilichomteremkia katika Qur-aan ilikuwa ni:

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ

Soma! Kwa jina la Mola wako aliyeumba – amemuumba mtu kutokana na pande la damu linaloning’inia! Soma na Mola wako ni Mkarimu kabisa. Ambaye aliyefunza kwa kalamu. Amemfunza mwanadamu yale asiyoyajua.”[1]

Kisha wahy ukakatika kwa kipindi fulani.

[1] 96:1-5

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 95
  • Imechapishwa: 12/09/2023