Du´aa wakati wa kuosha viungo vya wudhuu´

Swali: Baadhi ya watu wanategemea ile Hadiyth inayosomwa wakati wa kuosha kila kiungo?

Jibu: Hapana, haina dalili. Isipokuwa wakati wa kutawadha. Ataje jina la Allaah wakati wa kuanza kutawadha na ashuhudie mwishoni mwake. Haya ndio yamethibiti.

Swali: Je, ni lazima kuleta Basmalah wakati wa kutawadha?

Jibu: Kinachotambulika ni kwamba Tasmiyah inapendeza tu. Wako wanazuoni  wenye kuona kuwa ni lazima. Ahmad (Rahimahu Allaah) na jopo kubwa la wanazuoni wanaona kuwa inapendeza tu. Maoni ya pili yanasema kuwa ni lazima. Hata hivyo Hadiyth hiyo ni dhaifu. Hadiyth inayosema:

“Hakuna wudhuu´ kwa ambaye hakutaja jina la Allaah.”

Haafidhw [Ibn Hajar] amesema:

“… kwa mkusanyiko wake inafikia ngazi ya kuwa nzuri.”

Kwa hali yoyote muislamu hatakiwi kuiacha kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano. Kwa hivyo anatakiwa kuipatiliza mwanzoni mwa wudhuu´ iwapo ataikumbuka. Hata hivyo hakuna kitu juu yake endapo ataisahau au akawa ni mjinga juu yake.

Swali: Ailete katikati ya wudhuu´ pale ataposahau?

Jibu: Akiisahau aiseme katikati ya wudhuu´. Akiisahau indondoka kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22902/ما-الصحيح-من-اذكار-الوضوء
  • Imechapishwa: 12/09/2023