25. Jilbaab ilifaradhishwa kabla ya swalah ya ´iyd

2 – Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema tena:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika Madiynah, aliwakusanya wanawake wa Answaar katika nyumba kisha akawatumia ´Umar bin al-Khattwaab. ´Umar akasimama karibu na mlango na kuwatolea salamu ambapo wakaitikia salamu yake. Akasema: ”Mimi ni mjumbe wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenu nyinyi.” Wakasema: ”Karibu, ee mjumbe wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)!” Akasema: ”Je, mnakula kiapo juu ya kutomshirikisha Allaah na chochote, kutoiba, kutozini, kutowaua watoto wenu, msilete usingiziaji wa kashfa walioizua kati ya mikono yao na miguu yenu na wala hamtoasi katika yaliyo mema?” Tukajibu: ”Ndio.” ´Umar, ambaye alikuwa nje ya mlango, akanyoosha mkono wake, na sisi tukanyoosha mikono yetu kwa ndani. Kisha akasema: ”Ee Allaah! Shuhudia!”Kisha tukaamrishwa kutoka kwa ya swalah za ´iyd, wanawake wachanga na wenye hedhi. Vilevile tukaamrishwa kulisindikiza jeneza na tukaelezwa kwamba swalah ya ijumaa haitulazimu.” Nikamuuliza kuhusu usingiziaji wa kashfa walioizua na kuasi katika yaliyo mema. Akajibu: ”Ni maombolezo.”[1]

Kinacholengwa ni pale itakapobainika pindi tutapokumbuka kuwa Aayah:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا جَاءَكَ الْمُؤْمِنَاتُ يُبَايِعْنَكَ عَلَىٰ أَن لَّا يُشْرِكْنَ بِاللَّـهِ شَيْئًا وَلَا يَسْرِقْنَ وَلَا يَزْنِينَ وَلَا يَقْتُلْنَ أَوْلَادَهُنَّ وَلَا يَأْتِينَ بِبُهْتَانٍ يَفْتَرِينَهُ بَيْنَ أَيْدِيهِنَّ وَأَرْجُلِهِنَّ وَلَا يَعْصِينَكَ فِي مَعْرُوفٍ ۙ فَبَايِعْهُنَّ وَاسْتَغْفِرْ لَهُنَّ اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Ee Nabii! Wakikujia waumini wa kike kuahidiana nawe ahadi ya utiifu kwamba hawatomshirikisha Allaah na chochote wala hawatoiba wala hawatozini, wala hawatawaua watoto wao wala hawatoleta usingiziaji wa kashfa walioizua kati ya mikono yao na miguu yao na wala hawatokuasi katika mema, basi pokea kiapo chao cha utii na waombee msamaha kwa Allaah. Hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye Kurehemu.”[2]

iliteremshwa siku ya Ufunguzi[3] na baada ya Aayah ya Mtihani[4]. al-Miswar amesema kuwa Aayah ya Mtihani imeteremshwa siku ya Hudaybiyah. Maoni sahihi ni kwamba hayo yalitokea mwaka wa 06, kama alivosema Ibn-ul-Qayyim katika ”Zaad-ul-Ma´aad”.  Aayah inayoamrisha hijaab imeteremshwa mwaka wa 03. Kuna maon mengine yanayosema mwaka wa 05 wakati ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga kambi na Zaynab bint Jahsh, kama ilivyotajwa katika wasifu wake katika ”al-Iswaabah”.

Kwa hivyo ikafahamisha kuwa wanawake kuamrishwa kutoka kwenda kuswali swalah za ´iyd ilikuwa baada ya kufaradhishwa jilbaab. Kinachotilia nguvu hilo ijtihaad hiyo ni kitendo cha ´Umar aliyesimama nje ya mlango na hakuwaingilia wanawake ndani. Hapo na wakati huo ndipo aliwafikishia amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kutoka kwenda kuswali swalah za ´iyd. Kipindi hicho ilikuwa mwaka wa 06, punde tu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kurejea kutoka Hudaybiyah. Baada ya kuteremshwa Aayah ya Mtihani na Aayah ya kiapo kama tulivyotangulia kusema. Hapo ndio utafahamu maana ya maneno yake Umm ´Atwiyyah ”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipofika Madiynah” akikusudia kutoka Hudaybiyah na si kufika kwake kutoka Makkah.

[1] al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh al-Kabiyr” (1/1/361), Ahmad (6/408-409), al-Bayhaqiy (3/184) na adh-Dhwiyaa’ al-Maqdisiy katika ”al-Mukhtaarah” (1/104-105) kupitia kwa Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Atwiyyah, kutoka kwa bibi yake Umm ´Atwiyyah. Amesema:

”Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan wameipokea katika ”as-Swahiyh” zao.

Ismaa´iyl ametajwa na Ibn Abiy Haatim katika ”al-Jarh wat-Ta´diyl” (1/1/185) pasi na kumjeruhi wala kumsifu. Alikuwa mwenye kuaminika kwa mujibu wa Ibn Hibbaan. Imekuja katika ”at-Taqriyb” ya kwamba ni mwenye kukubaliwa. Mtu kama huyu inafaa kumtumia katika mapokezi yanayotilia nguvu, khaswa kwa kuzingatia kwamba adh-Dhahabiy amesema katika ”Mukhtaswar al-Bayhaqiy ” (2/133) kuwa cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Kukunja mkono kumetajwa katika ”as-Swahiyh” (4892) na ”al-Kabiyr” (24/182) ya at-Twabaraaniy kupitia njia kadhaa ambazo hakuna anayezipunga isipokuwa mwenye kufanya kiburi.

[2] 60:12

[3] Yamesemwa na Muqaatil. Tazama ”ad-Durr” (6/209).

[4] Amesema Jaabir, kama ambavo Ibn Marduuyah amepokea kutoka kwake. Tazama ”ad-Durr” (6/211).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 74-76
  • Imechapishwa: 12/09/2023