24. Hata baada ya hapo Maswahabah wa kike walikuwa wakionyesha nyuso zao

Pengine akawepo mwenye kusema kuwa Hadiyth zilizotajwa ziko wazi kabisa, lakini hata hivyo kuna uwezekano yakawa yametokea kabla ya kufurahishwa jilbaab. Kwa msemo mwingine si sahihi kuyajengea kama hoja isipokuwa baada ya kuthibitisha kuwa yametokea baada ya uwajibu wa jilbaab. Nitayajibu hayo kwa njia mbili:

Ya kwanza: Udhahiri wa dalili mbalimbali ni kwamba yametokea baada ya uwajibu wa jilbaab. Nitataja juu yake Hadiyth mbili:

1 – ´Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaamrisha wanawake kutoka kwa ajili ya kwenda kuswali ´iyd:

”Bado ni lazima kwetu kutoka kwenda ikiwa hana jilbaab?” Akajibu: ”Amvishe dada yake katika jilbaab zake. Ashuhudie kheri pamoja na waislamu.”[1]

 Hapa kuna dalili juu ya kwamba wanawake walikuwa wakienda kuswali swalah ya ´iyd wakiwa wamevaa jilbaab zao. Yule mwanamke ambaye alikuwa amepaka rangi kwenye mashavu alikuwa amevaa jilbaab.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 74
  • Imechapishwa: 12/09/2023