Kutundika picha msikitini na mahimizo ya kuwasaidia mafukara kwa kuweka picha zao

Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika picha msikitini?

Jibu: Haijuzu kutundika picha; si msikitini wala nyumbani. Hata nyumbani haijuzu. Ni mamoja picha ya mtu au ya mnyama.

Swali: Vipi kuhusu magazeti ya khabari?

Jibu: Hapana, haijuzu. Akiwa na picha afute kichwa chake na wala asiitundike juu ya ukuta.

Swali: Baadhi ya watu wanatundika picha za mafukara na wanaweka ujumbe wenye kusema “toeni swadaqah” na wanaandika Aayah zinazohimiza kutoa swadaqah.

Jibu: Hapana, haijuzu. Ahimize kutoa swadaqah bila picha. Ahimize mafukara kusaidiwa bila kuweka picha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22593/ما-حكم-تعليق-الصورة-في-المسجد
  • Imechapishwa: 07/07/2023