Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hana swalah kwa anayeswali peke yake nyuma ya safu.”

Je, hiyo maana kwamba swalah yake ni batili?

Jibu: Ndio, ndio udhahiri wa Hadiyth. ´Aliy bin Abiy Shaybah ameeleza:

”Tuliondoka mpaka tukafika kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Tukampa kiapo na tukaswali nyuma yake. Kisha tukaswali tena nyuma yake swalah nyingine. Baada ya kumaliza kuswali akamuona bwana mmoja anayeswali peke yake nyuma ya safu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama juu yake akimsubiri. Halafu akamwambia: ”Irudi swalah yako. Hana swalah ambaye anaswali nyuma ya safu.”[1]

Haya ndio madhehebu ya kikosi kikubwa. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) yeye anaona kuwa asipopata nafasi katika safu na asimpate mtu wa kupanga naye safu, basi inafaa kwake akaswali peke yake nyuma ya safu. Hoja yake ni kwamba wajibu unadondoka wakati wa kushindwa – na huku ni kushindwa. Lakini kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kinyume kutokana na Hadiyth hii.

[1] Ibn Maajah (1003). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (829).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 27/08/2023