19. Hadiyth “Yule atakayefanya mambo matano kwa imani ataingia Peponi… “

369 – Abud-Dardaa´ (Rahdiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

خمسٌ من جاء بهن مع إيمانٍ دَخَلَ الجنةَ: مَن حافظَ على الصلواتِ الخمسِ، على وُضوئهنّ، وركوعهنَّ، وسجودهنَّ، ومواقيتهنَّ، وصام رمضان، وحجّ البيتَ إنْ استطاع إليه سبيلاً، وآتى الزكاة طيّبةً بها نفسُه، وأدّى الأمانةَ

قيل: يا رسول الله! وما أداءُ الأمانةِ؟ قال

“الغُسل من الجنابة، إنَّ الله لم يَأمَنِ ابنَ آدم على شيءٍ من دينِه غَيرها”

“Yule atakayefanya mambo matano kwa imani ataingia Peponi: Mwenye kuhifadhi swalah tano, wudhuu´, Rukuu´, Sujuud na nyakati zake, akafunga Ramadhaan, akahiji Nyumba akiweza kuiendea, akatoa zakaah kwa moyo mkunjufu na akatekeleza amana.” Ikasemwa: “Ee Mtume wa Allaah, amana inatekelezwa vipi?” Akasema: “Josho kutokana na janaba. Allaah hajamkabidhi mwanadamu dini isiyokuwa hiyo.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/271)
  • Imechapishwa: 27/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy