Miongoni mwa faida za mitihani ni kwamba inapelekea kupata rehema na malipo ya Allaah makubwa:
“Warehemuni walioko ardhini atakurehemuni Aliye juu ya mbingu.”[1]
Miongoni mwa manufaa yake pia ni kuwa wale wanaopewa mitihani wanaingia katika kundi la wale wanaopendwa na wanaotukuzwa na mapenzi ya Mola wa walimwengu. Kwa sababu Yeye (Subhaanah) akiwapenda watu, basi huwapa mtihani.
Faida nyingine ni kwamba yule aliyepewa mtihani anaamka kutoka katika kughafilika kwake na kufanya mema na kutoa swadaqah yake. Tumepokea ya kwamba Ibraahiym bin al-´Abbaas as-Swawliy al-Kaatib amesema:
“Wakati al-Fadhwl bin Sahl alipokuwa mgonjwa Khurasaan, wakamtamania uzima na wakaanza kuzungumza. Walipomaliza, akawageukia watu na kusema: “Maradhi yana neema ambayo inatakiwa kwa wenye busara kuitambua. Yanafuta madhambi, yanapelekea kupata thawabu za subira, kuamka kutoka katika ughafilikaji, kuzikumbuka neema katika kipindi cha afya, kumfanya mtu kutubia na kuhimiza kutoa swadaqah – na katika mipango ya Allaah (Ta´ala) kuna kheri nyingi.” Wakasahau watu walichokuwa wanazungumza na wakaondoka na maneno ya al-Fadhwl.
[1] al-Albaaniy amesema:
”Ameipokea Abu Daawuud (4941), at-Tirmidhiy (1/350), Ahmad (2/160), al-Humaydiy (591), kupitia kwake al-Bukhaariy katika ”at-Taariykh” (64/574), Ibn Abiy Shaybah (8/526), al-Haakim (4/159) aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikianaa naye, al-Khatwiyb katika ”Taariykh Baghdaad” (3/260), al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (7/476) na Abul-Fath al-Khiraqiy katika ”al-Fawaa-id al-Multaqatwah” (222-223) Sufyaan bin ´Uyaynah, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Abu Qaabuus, mtumwa wa ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). at-Tirmidhiy amesema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh” (Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (2/596))
- Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 115-117
- Imechapishwa: 27/08/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)