Mke anaangusha baadhi ya haki zake

Swali: Je, inafaa kwa mke kuangusha baadhi ya haki zake za kindoa, kama vile matumizi au kulala usiku?

Jibu: Sawdah (Radhiya Allaahu ´anhaa) aliangusha haki yake na kumpa usiku wake ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ili Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asimtaliki. Kwa sababu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitaka kumwacha kwa sababu ya utuuzima wake, akakubali kumpa haki yake ´Aaishah ili abaki kuwa ni mke wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alitaka kubaki na utukufu huo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 27/08/2023