Swali: Nina mtihani wa kutokwa na upepo na khaswa wakati wa kutawadha. Sikaribii kumaliza wudhuu´ wangu isipokuwa natokwa na upepo. Je, niendelee kutawadha katika hali hii? Nifanye nini? Niswali vipi?

Jibu: Inaweza kuwa ni wasiwasi ambao hautakiwi kuujali. Shaytwaan anamtia wasiwasi wakati wa kutawadha. Anamuonesha kuwa ametokwa na upepo ili amshawishi. Asijalie. Anatakiwa kuendelea na kuswali.

Ama akiwa na uhakika kuwa ametokwa na upepo na akasikia sauti au akahisi harufu yake Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametupa alama) ya kuzingatia. Akihisi harufu au sauti atawadhe.

Na ikiwa hili ni jambo lenye kudumu kutokwa na upepo, huyu hadathi yake ni ya daima. Hivyo anatakiwa kutawadha kila pale ambapo anataka kuswali na kuswali hata kama atatokwa na upepo [wakati wa swalah].

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015