Swali: Kuna wanaowalingania watu katika mapinduzi na maandamano na kusema yanatofautiana mji kwa mji. Je, ni wajibu kutahadharisha kwa mtu mwenye kulingania katika mambo haya?

Jibu: Ndio. Hakuna kheri yoyote katika mapinduzi. Mapinduzi yanapelekea katika kumwaga damu na kuiharibu miji, kuangamiza mali na heshima. Mapinduzi hayajuzu. Lililowekwa katika Shari´ah ni Jihaad katika njia ya Allaah kwa masharti yake. Jihaad ambayo ni sahihi na ya Kishari´ah iliyowekwa. Kuhusiana na mapinduzi na vurugu, yote haya ni shari. Hayaleti kheri yoyote. Hayana matunda yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir-14340205.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015