Swali: Ni ipi hukumu ya kutoka nje ya msikiti baada ya adhaana kwa njia endelevu?

Jibu: Ikiwa anatoka kwa ajili ya manufaa, kwa mfano anaenda katika msikiti ambao anaswalisha au anatoka kwa ajili ya kutatua mahitaji yake na pengine hatorudi, ni kitu kinachofaa. Lakini muadhini akishaadhini na akawa hana udhuru unaokubalika katika Shari´ah, basi itambulike kuwa siku moja Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) alimuona mtu ambaye anafanya jambo hilo ambapo akasema:

“Kuhusu huyu hakika amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/
  • Imechapishwa: 11/06/2022