Kutoa Zakaat-ul-Fitwr kabla kwenda kwa taasisi ya Kiislamu ya kimataifa


Swali: Je, imewekwa katika Shari´ah kwa taasisi ya Kiislamu ya kimataifa kuchukua Zakaat-ul-Fitwr mwanzoni mwa Ramadhaan ili kuweza kufaidika nayo kwa kiasi kinachowezekana?

Jibu: Sionelei kufaa kufanya hivo. Wala sionelei kufaa kutoa Zakaat-ul-Fitwr nje ya nchi anayoishi mtu. Watu wanaoshi katika nchi hiyo wana haki zaidi ya Zakaat-ul-Fitwr hiyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Mu´aadh bin Jabal  wakati alipomtuma Yemen:

”Wafunze kwamba Allaah amefaradhisha juu ya mali yao zakaah itayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupewa mafukara wao.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/268)
  • Imechapishwa: 04/05/2021