Walii wa mwanamke alikuwa haswali


Swali: Nimemuoa mwanamke muislamu. Lakini walii wake mwanamke huyu ambaye alinioza alikuwa haswali kipindi aliponioza. Sikuwa nikijua kuwa ambaye haswali anazingatiwa kuwa ni kafiri. Hivi sasa nimekwishazaa mtoto na mwanamke huyu na nataka kujua kama ndoa yangu inazingatiwa ni sahihi au hapana?

Jibu: Midhali ulikuwa hujui ni mwenye kupewa udhuru. Lakini hivi sasa baada ya wewe kujua, ni lazima kwako kufunga ndoa upya. Ni jambo jepesi na si gumu. Funga ndoa upya mara nyingine na uache kubeba jukumu hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=olRgUbGftgg
  • Imechapishwa: 04/05/2021