3- Yanayoruhusu kwa mfanyaji I´tikaaf

Inaruhusu kwa aliyekaa I´tikaaf kutoka nje ya msikiti kwa yale mambo ambayo hakuna budi ayafanye. Mfano wa kutoka kwa ajili ya kula na kunywa akiwa hana mtu wa kumletea, kukidhi haja, kutawadha kutokamana na hadathi na kuoga janaba.

Anaruhusiwa kuzungumza na watu kwa mambo yenye faida na kuulizia hali zao. Ama kuzungumza mambo yasiyokuwa na faida na mambo yasiyokuwa na dharurah ni mambo yanayopingana na malengo ya I´tikaaf na yaliyosuniwa kwa ajili yake. Inaruhusu kwa baadhi ya wakeze na nduguze kumtembelea, wakamzungumzisha kwa kitambo fulani na akatoka katika I´tikaaf yake kwa ajili ya kuwaaga. Swafiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amekaa I´tikaaf ambapo nikamjia wakati wa usiku, nikamzungumzisha, halafu nikainuka na kugeuka. Akasimama kwa ajili ya kunisindikiza… “[1]

 Bi maana anamsindikiza nyumbani kwangu.

[1] al-Bukhaariy (2035) na Muslim (2175).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 169-170
  • Imechapishwa: 04/05/2021