Kuswali pasina kuadhini wala kukimu

Swali: Je, swalah inaathirika watu wakisahau kukimu na wakaswali? Ni mamoja ni mtu mmojammoja au ni kikosi cha watu?

Jibu: Akiswali mtu mmojammoja au kikosi cha watu pasi na kukimu swalah ni sahihi. Ni lazima kwa ambaye amefanya hivo kutubu kwa Allaah (Subhaanah). Vivyo hivyo wakiswali pasi na adhaana swalah ni sahihi. Kwa sababu adhaana na Iqaamah ni faradhi kwa baadhi ya watu. Ni mambo yanayotoka nje ya kiini cha swalah.

Ni lazima kwa ambaye ameacha kuadhana na kukimu kutubu kwa Allaah (Subhaanah) kutokamana na jambo hilo. Faradhi ambazo zinawalazimu baadhi ya watu wanapata dhambi wakiacha watu wote na inadondoka baadhi wakifanya hivo. Miongoni mwa mambo hayo ni adhaana na Iqaamah. Wakilitekeleza wanaotosheleza basi uwajibu na dhambi zinadondoka kutoka kwa waliobaki. Ni mamoja wako katika hali ya ukazi au safarini. Ni mamoja wako katika vijiji, miji na majangwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/359)
  • Imechapishwa: 23/09/2021