Swali: Baadhi ya waadhini wanasema “Laa ilaaha illa Allaah” au kuzungumza kabla ya kuanza kutoa adhaana. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi?

Jibu: Haijuzu kwa muadhini kuzidisha maneno yoyote katika adhaana. Haijalishi kitu kabla yake au baada yake. Kwa sababu adhaana ni ´ibaadah inayotekelezwa kwa mujibu wa dalili. Vivyo hivyo Iqaamah. Kwa hivyo ni wajibu kwa waadhini kujifungamanisha na yale iliyokuja nayo Shari´ah takasifu na watahadhari kutokamana na nyongeza ambazo hazikuwekwa katika Shari´ah na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) wala Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/360)
  • Imechapishwa: 23/09/2021