Swali: Tunapohama kutoka nyumba moja kwenda nyingine na kwa kuzingatia kwamba nyumba nyingi au sehemu kubwa ya nyumba huwa na sakafu iliyofunikwa kwa zulia, je, inajuzu mmoja wetu kuswali juu ya sehemu ambayo huenda ilimwagikiwa au kuenezwa pombe, kwa sababu hatujui kama waliokuwa wakiishi humo kabla yetu walikuwa waislamu?
Jibu: Msingi katika vitu ni kuwa ni twahara. Haihukumiwi kitu chochote kuwa ni najisi isipokuwa kwa kuwepo dalili inayoonyesha kwamba kitu hicho ni najisi na kwamba najisi hiyo iliyotajwa katika dalili ipo katika sehemu hiyo. Ikiwa mambo hayo mawili hayajathibiti, basi muislamu ataswali na swalah yake itakuwa sahihi.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/365)
- Imechapishwa: 26/11/2026
Swali: Tunapohama kutoka nyumba moja kwenda nyingine na kwa kuzingatia kwamba nyumba nyingi au sehemu kubwa ya nyumba huwa na sakafu iliyofunikwa kwa zulia, je, inajuzu mmoja wetu kuswali juu ya sehemu ambayo huenda ilimwagikiwa au kuenezwa pombe, kwa sababu hatujui kama waliokuwa wakiishi humo kabla yetu walikuwa waislamu?
Jibu: Msingi katika vitu ni kuwa ni twahara. Haihukumiwi kitu chochote kuwa ni najisi isipokuwa kwa kuwepo dalili inayoonyesha kwamba kitu hicho ni najisi na kwamba najisi hiyo iliyotajwa katika dalili ipo katika sehemu hiyo. Ikiwa mambo hayo mawili hayajathibiti, basi muislamu ataswali na swalah yake itakuwa sahihi.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/365)
Imechapishwa: 26/11/2026
https://firqatunnajia.com/kuswali-maeneo-ambayo-mtu-anadhani-kulimwagiwa-pombe/