Swali: Je, inajuzu kusoma Suurah Yaa Siyn kwa sauti ya juu msikitini au hapana?
Jibu: Haijuzu kwa yeyote kunyanyua sauti yake kwa kusoma Qur-aan msikitini, si kwa Suurah Yaa Siyn wala Suurah nyingine, si ndani ya swalah wala nje ya swalah. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka akawakuta watu wanaswali na wanasoma kwa sauti ambapo akasoma:
“Enyi watu! Kila mmoja wenu anamnong´oneza Mola Wake. Hivyo baadhi wasisome kwa sauti ya juu kwa wengine.”
Isitoshe kufanya hivo kuna kushawishana na kuudhiana.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (4/24)
- Imechapishwa: 22/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)