Kusoma nusu ”al-Insaan” na nusu ”as-Sajdah” Fajr ya siku ya ijumaa

Swali: Je, kusoma Suurah ”as-Sajdah” usiku wa ijumaa ni lazima kila wiki?

Jibu: Ni Sunnah ya kudumu kusoma Suurah ”as-Sajdah” na “al-Insaan” katika swalah ya Fajr siku ya ijumaa daima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akidumu juu yake. Si haramu ikiwa ataacha. Lakini hili ndilo Sunnah.

Swali: Je, wanaweza kuzigawanya?

Jibu: Hapana, Sunnah ni kusoma zote mbili. Kugawanya ni kinyume na Sunnah. Asome “as-Sajdah” katika Rak´ah ya kwanza na “al-Insaan” katika Rak´ah ya pili. Hii ndiyo Sunnah aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3512/حكم-قراءة-سورتي-السجدة-والانسان-في-صلاة-فجر-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 04/09/2026