Kusoma ndani ya maji na baadaye kuyauza kwa watu

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anasoma ndani ya maji kisha anayauza?

Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo. Ni sawa ikiwa anasoma kwa ajili ya mtu maalum kisha akampa nayo. Ama kuwauzia watu ni jambo halitakikani na halina dalili. Kunakhofiwa ikawa ni haramu. Si jambo zuri. Hapana vibaya kule kumsomea mtu maalum na akampa nayo hali ya kumsaidia. Kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsomea Thaabit bin Qays kisha akammiminia nayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22958/حكم-القراءة-في-الماء-وبيعه
  • Imechapishwa: 22/09/2023