Swali: Hadiyth inayosema:

“Watu aina sababu watafunikwa na kivuli cha Allaah siku ambayo kutakuwa hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake.”[1]

inafasiriwa na Hadiyth nyingine inayosema kuwa ni kivuli cha ´Arshi?

Jibu: Inafasiriwa kwa yote mawili. ´Arshi inayo kivuli na Allaah ana kivuli. Allaah ana kivuli ambacho hakuna anayejua namna yake isipokuwa Yeye (Jalla wa ´Alaa). Yamepokelewa yote mawili. Kumepokelewa kivuli cha ´Arshi na kumepokelewa pia kivuli Chake (Jalla wa ´Alaa).

[1] al-Bukhaariy (659) na Muslim (1031).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22954/معنى-الظل-في-حديث-السبعة-الذين-يظلهم-الله
  • Imechapishwa: 22/09/2023