Thawabu kwa kueneza ulinganizi kupitia sauti na maandishi yenye manufaa

Swali: Baadhi ya kanda za ulinganizi zinaathiri na zimekuwa ni sababu ya kuwaathiri watu wengi baada ya watu hao kusikiliza kanda hizo. Je, wale wanaosambaza kanda hizo na duka la rekodi wanashiriki katika kupata thawabu?

Jibu: Maoni yaliyo karibu zaidi na usawa – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba mwenye kanda hiyo anapata thawabu na anayeeneza kwa watu anapata thawabu zake. Wote wanalingania katika kheri. Ikiwa ni kanda nzuri na yenye manufaa, basi mwenye nayo anapata thawabu na mwenezaji ana thawabu mfano wa thawabu za kama yule ambaye anaeneza vitabu na kuwanakilia watu mihadhara. Aidha yule ambaye anaandika na kuvieneza kwa watu. Ni wenye kushirikiana katika ujira.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22962/من-يدخل-في-اجر-الشريط-والوساىل-الدعوية
  • Imechapishwa: 22/09/2023