Muda kwa ajili ya ulinganizi, na muda kwa ajili ya kutafuta riziki

Swali: Muda mwingi wa mlinganizi unatakiwa kuwekwa katika kujifunza elimu?

Jibu: Kutegemea na wepesi wake:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Basi mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Mlinganizi anaweza kuwa na haja ambayo hakuna wa kumtekelezea nayo. Vilevile pengine akawa na haja ili kuweza kuwahudumia familia yake. Kwa hivyo atenge wakati wa kujifunza elimu, kulingania na kutoa miongozo na wakati mwingine kwa ajili ya kutafuta riziki. Kutafuta riziki hakumzuii mtu kulingania kwa muuzaji, mnunuzi, mmiliki wa duka, anayempitia, anayesimama pamoja naye na kadhalika. Kujifunza elimu ni jambo jepesi kila mahali.

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22964/هل-يكون-جل-وقت-الداعية-للعلم
  • Imechapishwa: 22/09/2023