26. Safari ya usiku na ya kupandishwa mbinguni ilitokea wakati gani?

Swali 26: Safari ya usiku na ya kupandishwa mbinguni ilitokea wakati gani?

Jibu: Baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutimiza umri wa miaka khamsini. Safari ya usiku ilikuwa kutokea msikiti Mtakatifu kwenda msikiti wa al-Aqswaa. Kupandishwa mbinguni ilikuwa kutokea msikiti wa al-Aqswaa kwenda mpaka katika mkunazi wa mwisho kabisa. Alinyanyuliwa ujuu aloweza kusikia kalamu zikiandika na zaidi ya hivo. Akaona (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alama kubwa za Mola wake. Akafaradhishiwa swalah tano. Kisha akapambazuka akiwa Makkah. Asubuhi hiyohiyo akajiliwa na Jibriyl kumbainishia nyakati za swalah. Pindi alipowaeleza kuhusu Safari ya usiku basi iliongezeka imani ya wale walioamini na ukaidi na dhuluma za makafiri zikazidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 22/09/2023