Kusoma du´aa kwenye karatasi ndani ya swalah

Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah kabla ya Tasliym mtu akaandika Du´aa na akaishika na kuzisoma?

Jibu: Azihifadhi na asiziandike. Ni tatizo kuzisoma ndani ya Swalah. Baadhi ya wanachuoni wamefikia kusema hata ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah kusoma ndani ya msahafu. Haijuzu kusoma ndani ya msahafu kwenye Swalah midhali hakuna haja. Azihifadhi Du´aa anazoweza na asiandike kwenye karatasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340127.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015