Swali: Ni kiwango kipi kwa yule mwenye kuacha kuswali anakufuru? Je, yule mwenye kuacha swalah moja tu anakuwa kafiri au inahitajia kwa mtu kudumu katika kuziacha?

Jibu: Mwenye kuacha swalah moja kwa kukusudia anakufuru. Ni wajibu kutubu kwa Allaah na asilimu upya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema yule mwenye kusahau swalah au akapitikiwa na usingizi aiswali pale atapokumbuka. Hakutaja kwa yule mtu mwenye kuacha kwa kukusudia kuwa ailipe. Hii ni dalili inayoonyesha kuwa ni lazima kwake kutubu na kuhifadhi swalah upya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340127.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015