Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Niko mbali na muislamu anayeishi kati ya washirikina.”

Je, hili linahusu pia mtu anafanya utalii katika miji ya makafiri?

Jibu: Ndio. Haijuzu kusafiri katika miji ya makafiri pasi na haja. Utalii sio haja. Haja ni kwa mfano matibabu ambayo hayapatiki isipokuwa huko, biashara na mikataba ya biashara na makampuni, masomo yasiyopatikani isipokuwa huko ambayo twahayahitajia, kulingania katika dini ya Allaah. Ama kusafiri kwa ajili ya utalii na kuishi huko haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340127.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015