Swali: Je, mtu aigawanye as-Sajdah katika swalah ya Fajr kati ya Rak´ah mbili?

Jibu: Hapana. Sunnah ni yeye asome as-Sajdah katika Rak´ah ya kwanza na al-Insaan katika Rak´ah ya pili. Hii ndio Sunnah.

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa ni Bid´ah?

Jibu: Hapana, ameenda kinyume na Sunnah. Si lazima iwe Bid´ah. Ni kwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23526/هل-تقرا-السجدة-في-صلاة-الفجر-في-ركعتين
  • Imechapishwa: 07/02/2024