Ada yake imekorogeka baada ya kuweka kitanzi cha uzazi wa mpango

Swali: Mwanamke akiweka kitanzi kisha akatokwa na damu ndogo inakuwa ni damu ya ugonjwa au hedhi?

Jibu: Atarudi katika ile kawaida yake. Ile damu inayotoka wakati wa kupata ada yake ataacha swalah. Na Ile damu inayotoka wakati usiyokuwa wa kupata ada yake itakuwa ni damu ya ugonjwa na damu ya kawaida.

Swali: Ada yake imekorogeka kwa sababu ya kitanzi hiki?

Jibu: Haijalishi kitu. Arudi katika ile kawaida yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23541/حكم-الدم-اليسير-الناتج-عن-اللولب-للنساء
  • Imechapishwa: 07/02/2024